Klabu ya Real Madrid imeulizia bei ya Mshambuliaji kutoka nchini Argentina na Klabu ya Inter Milan ya Italia Lautaro Martinez, ikiwa ni katika harakati za kutaka kumsajili katika dirisha hili la usajili Ulaya ili kwenda kuboresha eneo la ushambuliaji.

Madrid inamuangalia Lautaro mwenye umri wa miaka 25, kama mbadala wa Eden Hazard ambaye ameondoka katika dirisha hili sambamba na Karim Benzema aliyemalizana na wababe hao wa Santiago Bernabeu kisha kutimkia zake Uarabuni.

Lautaro ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika ifikapo 2026, amewahi kuhitajika sana na FC Barcelona katika madirisha kadhaa yaliyopita ya usajili, lakini ilishindikana kuondoka huko Italia.

Inadaiwa kwamba Inter Milan itahitaji walau Euro 70 milioni ili kumuuza mchezaji huyo ambaye amekuwa moto katika kikosi chake, lakini kiasi hicho cha fedha kinaweza kupungua.

Watoto waonja mafanikio miaka 60 ya  JTK
Usajili wa Azam FC washangaza