Uongozi wa Young Africans, umeweka wazi kuwa utakutana na wapinzani wao kwenye Ngao ya Jamii na kuonyesha ubora wa wachezaji ambao watakuwa ndani ya kikosi hicho.
Young Africans walitwaa taji la Ngao ya Jamii 2022/23 kwa ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Young Africans 2-1 Simba SC huku mabao ya Young Africans yote yalifungwa na Fiston Mayele na lile la Simba SC ni Pape Sakho.
Msimu wa 2023/24 ni mfumo mpya utatumika kusaka mshindi wa taji la Ngao ya Jamii na timu nne zitashiriki Simba SC, Singida Fountain Gate na Young Africans wenyewe itakuwa Tanga, Uwanja wa Mkwakwani.
Afisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe, amesema kuwa wanatambua utakuwa mfumo tofauti kwenye ushiriki hivyo wanawasubiri wapinzani wao.
“Wapinzani wetu tunakwenda kukutana nao ni mfumo tofauti utakuwa hivyo tunakwenda kukutana nao kwenye ushindani tukiwa na wachezaji wetu wapya na wale wa zamani.
“Tulitwaa taji la Ngao ya Jamii tulipokutana na watani zetu tunakwenda kukutana nao kwa mara nyingine tena kwenye mchezo wetu wa Ngao ya Jamii tutafanya kweli.
“Kuna wale wengine Singida Fountain Gate hii imebadili jina tunakutana nayo hatuna mashaka hilo kwetu halipo shida kwa kuwa tupo imara,” amesema Kamwe.