Kiungo kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum Abdallah, rasmi ameanza mazoezi akiwa sambamba na Kikosi cha Azam FC leo Alhamis (Julai 06) katika viunga vya Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

Feisal amesajiliwa Azam FC akitokea kwa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, baada ya kuvutana kwa muda mrefu na uongozi wa klabu hiyo katika suala la kuvunjwa kwa mkataba wake.

Picha zilizowekwa katika kurasa za Mitandao ya Kijamii za Klabu ya Azam FC zimemuonesha Feisal akiwa katika mazoezi ya wenzake, huku akionekana mwenye furaha.

Azam FC imepanga kuweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya 2023/24 nchini Tunisia, na inatarajia kuondoka jijini Dar es salaam Jumapili (Julai 09).

Wananchi wapewa nguvu ujenzi kituo cha Afya
Daniel Cadena aibukia mitaa ya Msimbazi