Maisha ya Angel Di Maria barani Ulaya yameingia kwenye mzunguko mwingine baada ya winga huyo kuamua kujiunga tena na Klabu ya Benfica ya Ureno akiwa mchezaji huru.

Di Maria katika maisha yake ya kwanza kucheza soka Ulaya alisajiliwa na Benfica ambako aliichezea kati ya mwaka 2007 na 2010.

“Karibu nyumbani, Di Maria!” Klabu hiyo ilisema baada ya video iliyotangaza kusajiliwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 ambaye kwa mujibu wa ripoti, amekubali kusaini mkataba wa mwaka mmoja.

Katika maisha yake ya kwanza Di Maria Ulaya akiwa na mabingwa hao wa Ureno ndio yaliyomfanya kuonwa na wababe wa Hispania, Real Madrid.

Alijiunga nao ambako alishinda nao taji la ligi, mataji mawili ya ndani na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Muargentina huyo alikaa msimu uliopita akiwa na Juventus ya Ligi Kuu Italia, Serie A, baada ya miaka saba ya mafanikio akiwa na Paris Saint-Germain.

Di Maria huko Ureno ataungana na rafiki yake wa karibu, Nicolas Otamendi raia mwenzake wa Argentina ambaye walishinda nae kombe la Dunia.

Mayele amshauri Fei toto, awatuliza mashabiki
Serikali yaja na mkakati motisha kwa Wanafunzi