Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza Mawaziri wenye dhamana na lugha ya Kiswahili, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mawaziri wa Elimu, kwa pande zote za Tanzania Bara na Zanzibar kuweka mikakati iliyo wazi ya kukuza lugha ya Kiswahili na kuweka motisha kwa vijana wanaofanya vizuri shuleni.

Majaliwa ameyasema hayo wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Kiswahili duniani katika ukumbi wa Chuo cha Polisi, Ziwani Zanzibar na kuongeza kuwa Watanzania wanayo nafasi ya kupata ajira ya Ualimu kwenye nchi mbalimbali Duniani, ambazo zimeingiza  somo la Kiswahili katika mitaala yao.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Amesema, mamlaka zinazoshughulika masuala ya ajira ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi), zinatakiwa kuhakikisha wanaandaa na kuratibu mipango ya kutafuta nafasi za kufundisha lugha ya Kiswahili katika mbalimbali ili Watanzania waweze kwenda kutumia fursa hizo.

Hata hivyo, Majaliwa ameongeza kuwa, “Marais Wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussein Ali Mwinyi wamesema mara kadhaa, tuhakikishe Kiswahili kinakuwa na kuwanufaisha Watanzania hovyo tujitahidi kuweka mazingira wezeshi ili kufanikisha lengo husika.”

Angel Di Maria akubali kurudi nyumbani
Masoud Djuma: Hapa Simba SC imepata mtu