Waziri wa Nishati, January Makamba amesema Mawaziri sita kutoka Tanzania na Zambia watakutana kwenye kikao kazi kitakachojadili ushirikiano baina ya nchi zao juu ya ulinzi na usalama wa Bomba la Mafuta la TAZAMA na sekta ya nishati.

Kikao kazi hicho, kitatathmini utekelezaji huo kama ilivyokubalika katika kikao cha kwanza cha Wizara hizo tatu kilichofanyika Desemba, 2022 jijini Dar es Salaam baada ya Serikali ya Zambia kuamua kutumia bomba hilo kusafirisha mafuta safi badala ya mafuta ghafi (crude oil).

Amesema, Bomba la TAZAMA lina urefu wa KM 1,710 kutoka Kigamboni – Dar es Salaam hadi Indeni – Ndola Zambia, na changamoto kubwa iliyopo ni ulinzi na usalama wa bomba hilo baada ya kuanza kusafirisha mafuta yaliyosafishwa badala ya mafuta ghafi.

Waziri wa Nishati, January Makamba wakati akiongea na vyombo vya Habari.

Aidha, Makamba amesema katika kikao cha kwanza ilikubalika mikakati mbalimbali itekelezwe ikiwemo ushirikishwaji wa wanavijiji katika sehemu ambapo bomba linapita na  ilikubalika kuwa mikakati mbalimbali itekelezwe ikiwemo ushirikishwaji wa wanavijiji katika sehemu ambazo bomba linapita.

Kwa upande wa Tanzania kikao hicho kitaongozwa na January Makamba – Waziri wa Nishati na kuhudhuriwa na Innocent Bashungwa – Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Mhandisi Hamad Y. Masauni – Waziri wa Mambo ya Ndani huku upande wa serikali ya Zambia, watakutana Ambrose L. Lufuma- Waziri wa Ulinzi,  Jacob J. Mwiimbu- Waziri Mambo ya Ndani na Peter C. Kapala- Waziri wa Nishati.

Mahrez atengewa mshahara mnono Saudi Arabia
Simon Msuva: Kibabage ana kazi kubwa Young Africans