Mchakato wa bomba la Mafuta la  TAZAMA lililojengwa miaka ya 1960, ambalo lilikua likisafirisha mafuta ghafi Nchini Zambia umebadilisha mfumo utakao safirisha mafuta yaliyosafishwa na sasa linasafirisha mafuta ya Dizeli na sio mafuta ghafi kama awali.

Waziri wa Nishati, Januari Makamba ameyasema hayo na kuongeza kuwa kufuatia kuanza kwa usafirishaji huo, hali na mahitaji ya usalama wa bomba hilo imeongezeka kwani watu hushawishika kutoboa na kuchukua Dizeli. Amesema, ‘tumeshafanya mkutano wa kwanza mwaka jana tuliweka makubaliano ya kuweza kulilinda bomba hili lenye urefu wa KM 1,710 kutoka Kigamboni – Dar es salaam hadi Indeni – Ndola Zambia.”

Waziri wa Nishati, Januari Makamba.

Hata hivyo, Waziri Makamba amesema,  “kikao tunachokutana kitapokea taarifa ya utekelezaji wa bomba hilo na mapendekezo ya ujenzi wa bomba jipya katika mkuza huo, bomba hili limejengwa muda mrefu na lina kipenyo chembaba biashara ya mafuta imekua na mahitaji ya mafuta yamekua zaidi.”

Ameongeza kuwa, “kuna haja ya kujenga bomba pana na jipya litakalosafirisha pia bidhaa nyingine zaidi ya Dizeli, Serikali zote mbili zimekua zikiongea kuhusu biashara hii ya mafuta na ujenzi wa bomba jipya la gesi ili kuiuzia Zambia Gesi.”

Hatua hiyo inatokana na ushirikiano mzuri kati ya Tanzania na Zambia na mwendelezo wa mahusiano mema unaofanywa na Viongozi Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Hakainde Hichilema, Rais wa Jamhuri ya Zambia kama yalivyoasisiwa na Viongozi hao wa kwanza Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere na Hayati Kenneth Kaunda.

Kagera Sugar kupitisha panga zito
Mahrez atengewa mshahara mnono Saudi Arabia