Chama cha Mapinduzi – CCM, kimemfuta uanachama mtoto wa muasisi wa Zanzibar, Sheikh Abeid Aman Karume, Balozi Ali Karume.

Balozi Karume anafutiwa uanachama wa CCM, ikiwa ni siku chache tangu apewe onyo na kuwekwa chini ya uangalizi, kutokana na kauli zake tata zilizodaiwa kuzitoa na kuidhalilisha CCM.

Mtoto wa muasisi wa Zanzibar, Sheikh Abeid Aman Karume, Balozi Ali Karume.

Kikao hicho cha kumfuta uanachama Balozi Karume, kimefanyika usiku wa kuamkia Julai 8, 2023 chini ya Katibu wa Mkoa wa CCM, Amina Mnacho.

Hata hivyo, hakuna tamko lolote la Balozi Ali Karume ambaye aliwahi kuweka nia ya kugombea Urais mwaka 2020, kuhusu hatua hiyo iliyochukuliwa na CCM.

Gabiel Jesus: Guardiola alinitoa machozi Man City
Wachezaji Azam FC waongezewa dozi