Imeelezwa kuwa Klabu ya Chelsea itatakiwa kutoa zaidi ya Pauni 100 milioni ili kuipata huduma ya kiungo wa Brighton na Ecuador, Moises Caicedo, katika dirisha hili la usajili.

Caicedo ambaye mkataba wake na Brighton unamalizika 2027, huduma yake inahitajika na timu nyingi Ulaya ikiwa pamoja na Manchester United.

Hata hivyo inadaiwa kuwa Kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino amewaambia mabosi kwamba anahitaji huduma ya Caicedo mwenye umri wa miaka 21 kwa gharama yoyote ili akacheze sambamba na Enzo Fernandez.

Awali ilielezwa Kiungo huyu angepatikana kwa kiasi cha pesa ambacho kisingezidi Pauni 80 hadi 90 milioni, lakini Brighton wamepandisha bei baada ya kuona Declan Rice ameuzwa zaidi ya Pauni 100 milioni.

Chelsea ina upungufu mkubwa eneo la kiungo ambalo limeondokewa na mastaa kibao ikiwemo N’Golo Kanté, Mateo Kovacic na Ruben Loftus-Cheek.

Kiungo huyu wa kimataifa wa Ecuador msimu uliopita alicheza mechi 43 za michuano yote na kufunga bao moja huko England.

Rais Samia mgeni rasmi maadhimisho miaka 60 ya JKT
Juma Said Nyosso kurudi Kagera Sugar