Mtu mmoja, Zakaria Miti mkazi wa Sabasaba Manispaa Morogoro anayekadiriwa kubwa na umri wa miaka 80 amefariki, baada ya nyumba aliyokuwa akiishi kuungua moto asubuhi ya leo Julai 11, 2023.

Akisimulia tukio, mtoto wa Marehemu Prosper Zakaria amesema katika nyumba hiyo walikua wakiishi watu wanne wakiwemo baba yake, na wakati tukio linatokea mama yake alikua kanisani na wanafunzi walikua shule hivyo alibaki marehemu ambaye alikua ni mlemavu wa viungo.

Amesema baada ya tukio walitoa taarifa Polisi na kusema, “walifika wakitembea kwa miguu wengine wakipanda bodaboda kisha kuchukua maji nyumba za jirani kwa kutumia ndoo kisha kuanza kuzima moto huo lakini jitihada zao hazikuzaa matunda.”

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Morogoro, Emanuel Ochieng amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema changamoto iliyosababisha jeshi hilo kuchelewa kwenye tukio hadi nyumba kutekeleza gari ambalo linatumiwa ni bovu na lipo kwenye matengenezo jambo ambalo askari wa zimamoto wamelazimika kutembea kwa miguu hadi eneo la tukio.

Kutokana na changamoto hiyo mbunge wa jimbo la Morogoro Abdulaziz Abood amesema atagharania matengenezo ya gari hilo ili lianze kufanya kazi.

Viongozi wa upinzani wakaidi agizo la Serikali
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 12, 2023