Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema moja ya vikwazo vikubwa vya maendeleo barani Afrika ni pamoja na janga la rushwa ambalo linadhoofisha mifumo kitaasisi na kuathiri mipango na mikakati ya kujikomboa kiuchumi.

Ameyasema hayo jijini Arusha katika kilele cha maadhimisho ya siku ya kupambana na rushwa barani Afrika yaliyokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 20 tangu kusainiwa mkataba wa Umoja wa Afrika wa kupambana na rushwa.

Amesema, “Rushwa inaadhoofisha mifumo ya kitaasisi na kuathiri mipango, vitendo vya rushwa haviiishii kwenye mipaka ya kitaifa kwa kutambua hili ni muhimu kwa nchi za Afrika kushirikiana katika mapambano haya kwa kupeana misaada ya kisheria pamoja na ushirikiano wa kiufundi.”

“Wala rushwa wanapaswa kufahamu kuwa nchi zetu si vichaka vya kuficha fedha zinazotokana na rushwa au kufuga wala rushwa, tunataka dunia nzima ifahmu kwamba Afrika si mahali salama kwa wala rushwa na hilo lionekane kwa vitendo kupitia hatua tunazozichukua na si mikutano, makongamano na maneno peke yake,” ameongeza Rais Samia.

Aidha, amewataka viongozi kutafakari na kuchambua kwa dhati maswala ya rushwa ili kubainisha changamoto au vikwazo vya mapambano hayo na kuchukua hatua muafaka na kwamba Serikali inaendelea kuimarisha Taasisi ya rushwa TAKUKURU kwa upande wa bajeti na mifumo ili kuleta ufanisi katika mapambano dhidi ya rushwa.

Hata hivyo amebainisha kuwa, Serikali imeweka zaidi katika matumizi ya mifumo ya TEHAMA inayosaidia kupunuza mawasiliano ya ana kwa ana katika kutoa huduma kama michakato ya zabuni usajili wa biashara na namba na namba ya mlipa kodi ili kupubguza mianya ya rushwa.

Serikali yafurahia maendeleo kituo cha Sayansi Tanga
Waarabu wa Saudia wahamia kwa Pogba