Boniface Gideon – Tanga.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda ameonesha kufurahishwa na Maendeleo makubwa ya kuinua Sayansi mkoani Tanga baada ya ujio wa Kituo cha Sayansi Tanga jiji cha STEM PARK kilicho chini ya usimamizi wa Project Insipire na kusema Serikali inachakata kujenga kituo kikubwa cha Sayansi na Teknolojia Mkoani Dodoma.

Waziri Mkenda ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea kituo cha Sayansi cha Stem Park kilichopo Jijini Tanga, mpango ambao alisema utasaidia kumaliza tatizo la wanafunzi kutopenda masomo ya sayansi, na kwamba , kituo cha Dodoma kitatumiwa na viongozi wa serikali kama mfano utakaosaidia vituo vya aina hiyo kujengwa maeneo mbalimbali nchini ili kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya sayansi.

Mkurugenzi wa Kituo cha Sayansi Mkoani Tanga – Tanga Stem Park, Dkt Lwidiko Edward (Kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda wakati wa ziara yake ya siku mbili, aliyekipongeza Kituo hicho kwa kusaidia kuinua Sayansi mkoani Tanga.

Amesema, “Ujio wa Kituo hiki umesaidia Sana tatizo la Wanafunzi kutokupenda masomo ya Sayansi,tunawapongeza wote waliofanikisha Ujenzi wa Kituo hiki lakini Mpango wa Serikali nikuongeza vituo vingi zaidi vya Sayansi na katika kufanikisha hili tutashirikiana na Project Inspire kujenga Kituo kikubwa mkoani Dodoma.”

“Dodoma ni katikati ya nchi yetu halafu pale wabunge, mawaziri wenzangu na watu mbalimbali wakuu wa mikoa nitapenda watembelee pale waone nini kinaweza kufanyika vituo hivi vinapaswa kujengwa kila mikoa najua haitafikia wanafunzi wote vitu vyote hivi ni matumda ambayo yanapatikana kkirahisi, ” amesema Waziri Mkenda.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Project Insipire, Lwidiko Edward alisema kituo hicho kinawatengeneza Wanafunzi kwenye masomo ya sayansi kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo kujifunza kwa Vitendo na kuandaa mazingira yanayotoa hamasa ya kusoma,

“Kituo hiki mpaka Sasa hivi kimewanufaisha maelfu ya Wanafunzi kutoka Mikoa mbalimbali Nchini,Bara na Visiwani,tunafundisha kwa vitendo zaidi kwakutumia mbinu na Vifaa vya kisasa zaidi vya Sayansi, hivyo tunawaandaa Wanasayansi mahiri wa baadae,” alisema Edward.

Azam FC kujipima mara tano Tunisia
Rushwa inadhoofisha mifumo - Rais Samia