Kocha Mkuu wa Arsenal Mikel Arteta ameongeza wachezaji watatu kutoka akademi ya Arsenal tayari kwa maandalizi ya msimu wa 2023/24 huko Ujerumani.

Ethan Nwaneri, Myles Lewis-Skelly na Reuell Walters, wamesafiri na timu na watafanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha The Gunners.

Mechi ya kwanza ya The Gunners ya kujiandaa na msimu mpya itakuwa kesho Alhamisi (Julai 13) watakapomenyana na timu ya daraja la pili ya Ujerumani, FC Nurnberg.

Baada ya hapo, watasafiri kwenda Marekani ambako watamenyana na MLS All-Stars, Manchester United na FC Barcelona, kabla ya kurejea Emirates kwa ajili ya kumenyana na AS Monaco.

Kiungo wa kati, Lewis-Skelly mwenye umri wa miaka 16 tayari ni mchezaji wa kawaida kwa timu za U21 na U18, wakati beki wa kulia, Walters, 18, aliwahi kukaa benchi kikosi cha wakubwa na Nwaneri anarekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kucheza Premier msimu uliopita akiwa na miaka 15 na siku 181.

Leonardo amuwashia moto Mbappe
Hamsemi mazuri ya nchi, mnapotosha - Silaa