Mshambuliaji Kylian Mbappe ameambiwa anaweza kuondoka Paris Saint-Germain huku akisindikizwa na maneno ya kushtua kutoka kwa mkurugenzi wa zamani wa michezo Leonardo Araújo.

Mei 2022, Leonardo alifutwa kazi na Paris Saint-Germain licha ya kufanikiwa kumshawishi Neymar kubaki Paris.

Mbappe na PSG kwa sasa wako kwenye mvutano kuhusu mkataba, huku mchezaji huyo akiweka wazi kuwa hataongeza mkataba wake wa sasa ambao unaisha mwaka 2024 na ataondoka bure punde tu ukiisha.

Hii imepelekea mabingwa hao wa Ligue 1 kumpa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, muda maalum wa kuhakikisha anafanya maamuzi ya kuongeza mkataba au auzwe majira haya ya joto.

Kufuatia sakata hilo, ametema cheche huku akiweka wazi kuwa PSG inaweza kubea Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya bila uwepo wa Mbappe.

“PSG ilikuwepo kabla ya Mbappe na itakuwepo baada yake.

“Timu tano zimeshinda Ligi ya Mabingwa kwa miaka sita. Hakuna hata mmoja wao aliyekuwa na Mbappe, hivyo inawezekana kabisa kushinda bila yeye,” Leonardo aliiambia L’Equipe.”

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 13, 2023
Watatu waongezwa kambi ya Arsenal