Kocha Mpya wa Klabu ya Al Ettifag, Steven Gerrard anadaiwa kuwasilisha jina la Mshambuliaji kutoka nchini Gabon na klabu ya Chelsea Pierre-Emerick Aubameyang akitaka asajiliwe katika dirisha hili.

Auba ambaye pia amekuwa akihusishwa kuwa kwenye mpango wa kutaka kurudi FC Barcelona, mkataba wake na Chelsea unamalizika mwakani.

Mshambuliaji huyo anataka kuondoka kwa sababu hapati nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea, hivyo anahitaji changamoto mpya kwenye timu ambayo anaona atapata nafasi ya kucheza.

Kumekuwa na ofa nyingi kutoka baadhi ya timu barani Ulaya lakini mzigo wa pesa ambao Al Ettifaq inadaiwa kuuweka meza ni unaonekana kuwa kumshawishi zaidi atue zake Saudia kuliko kubakia barani Ulaya.

Aubameyang ambaye ana umri wa miaka 34, msimu uliopita alicheza mechi 22 za michuano yote na kufunga mabao matatu.

Raila rafiki wa Wajackoya 'mabangi' unatarajia nini - DP Gachagua
Waziri Ummy atangaza malipo ya Madaktari