Kiungo wa kati kutoka nchini Brazil na Klabu ya Manchester United, Frederico Rodrigues de Paula Santos ‘Fred’ anafikiria mustakabali wake pale Old Trafford huku klabu kadhaa zikianza kumsukia mipango ya kumsajili.

Kiungo huyo alisajiliwa na Manchester United Juni 2018, lakini amekosa nafasi chini ya wa sasa, Erik ten Hag katika miezi ya mwisho ya msimu uliopita, akianza mechi mbili pekee za Ligi Kuu England chini ya Mholanzi huyo baada ya timu hiyo kufungwa 7-0 na Liverpool Uwanja wa Anfield.

Usajili wa United wa Mason Mount mwezi huu umemsukuma Fred, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 30, kutathmini chaguo lake huku nafasi ya kikosi cha kwanza ikiwa ni ngumu kupatikana katika msimu mpya.

Ten Hag pia angependa kusajili kiungo mwingine kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa, huku Sofyan Amrabat wa Fiorentina akitakiwa.

Fred inaonesha wazi hayumo kwenye mipango ya muda mrefu ya United na klabu iko tayari kumruhusu aondoke kwa bei inayofaa wakati wa dirisha hili la uhamisho.

United wana matumaini kwamba wanaweza kurejesha kati ya paumi milioni 20 hadi 25 katika mauzo yoyote yanayoweza kufanyika.

Fulham inavutiwa nae, lakini wanamthamini Fred kwa chini ya pauni milioni 15- chini kabisa ya hesabu ya sasa ya United.

Mchezaji huyo alionekana akizungumza na kocha wa Fulham, Marco Silva nje ya Old Trafford baada ya mechi ya mwisho ya ligi msimu uliopita, ambapo pande hizo mbili zilikutana.

Fred amebadilisha wakala hivi karibuni na ana chaguzi zingine za kuondoka – huku klabu za Saudi Arabia zikiwa vinawania kumsajili huku vikiendelea kufagia wachezaji wa hadhi ya juu kutoka barani Ulaya.

Mchezaji mwenzake Fred wa zamani wa United, Paul Pogba anavutiwa sana na Al Ahli na Al Ittihad, ambapo N’Golo Kante na Karim Benzema ni miongoni mwa majina makubwa ambayo tayari yamechukua hatua hiyo.

Inafahamika kuwa AS Roma ya Jose Mourinho ilizungumza na wawakilishi wa Fred Mourinho alimsajili Fred kule United wakati wa enzi yake kama kocha ingawa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 bado hajafanya uamuzi wa wapi pa kucheza.

GGML KiliChallenge - 2023: Dkt. Kikwete kuwaaga wapanda mlima
NECTA yatangaza matokeo kidato cha sita, ufaulu waongezeka