Uongozi wa Klabu Bingwa nchini England Manchester City umecheka uvumi kwamba, wanaweza kuwa tayari kuachana na mshambuliaji, Julian Alvarez msimu huu wa joto.
FC Bayern Munich wameonyesha nia ya kutaka kumsajili Alvarez, ambaye alikuwa na kibarua kizito cha kumsaidia Erling Haaland kwenye Uwanja wa Etihad msimu uliopita.
Alvarez mwenye umri wa miaka 23, ambaye anaonekana kuwa mmoja wa washambuliaji bora chipukizi wa mchezo huo, alifunga mabao 17 katika mechi 49 katika msimu wake wa kwanza pale Manchester na sasa ametajwa kuwindwa na klabu kadhaa Ulaya.
Hata hivyo, vyanzo vimethibitisha kwa 90min kwamba City wamefurahishwa na mchango wa Alvarez na hawana mpango wa kumpoteza msimu huu wa joto, huku mshindi huyo wa Kombe la Dunia pia anafahamika kuwa na furaha katika klabu hiyo.
Hisia za Alvarez kuhusu hali yake ndani ya City ziliwekwa wazi Machi, aliposaini mkataba mpya wa miaka mitano na bado kuna nia ya kuendelea kufanya kazi pamoja pale Etihad.
FC Bayern Munich wamefahamishwa vyema kwamba hakuna nafasi ya kumsajili Alvarez msimu huu wa joto.