Klabu ya Chelsea iatapata hasara ya Pauni Milioni 97.5 (Sh bil 307.2) kwa Mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji Romelu Lukaku iwapo watakubali ombi la Inter Milan kumnunua mchezaji huyo.

Inter Milan wameripotiwa kuwasilisha ofa mpya kwa ajili ya Lukaku lakini ina maana kwamba Chelsea watapata hasara kubwa kwa nyota huyo wa Pauni Milioni 97.5.

Inter wamekataliwa ofa moja ya kutaka kumnunua mchezaji huyo lakini sasa wamepeleka ofa yao ya pili yenye thamani ya Pauni Milioni 25.7, hii ni kwa mujibu wa mwandishi wa habari za usajili, Fabrizio Romano.

Hata hivyo Chelsea wanataka takriban Pauni Milioni 40 lakini wanaweza kulazimika kuridhika na bei ndogo huku Lukaku akikataa kurejea mazoezini kama sehemu ya kushinikiza kuuzwa Inter ambako anafurahia maisha yake kisoka.

Morocco kuirudisha kimataifa Geita Gold
Twaha Kiduku: Dullah Mbabe atambamiza Katompa