Jeshi la Polisi nchini, limekemea kitendo cha kuibuka makundi ya watu, Kampuni Binafsi za Ulinzi na baadhi ya Walinzi wa Viongozi wanaovaa mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na Usalama katika siku za karibuni.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP. David Misime amesema sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kifungu cha 178, inakataza mtu ambaye si askari wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama kuvaa sare za majeshi sambamba na ile ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1970 kifungu cha 6.

Amesema, Jeshi la Polisi Tanzania linawataka wale wote wenye tabia ya kuvaa mavazi yanayofanana na sare za majeshi ya ulinzi na usalama kinyume na sheria za nchi, kuacha tabia hiyo mara moja kwani halitasita kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Aidha, Misime ameongeza kuwa Jeshi la Polisi Tanzania linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili kuendelee kuiweka nchi salama.

Yara kushughulikia changamoto usambazaji wa Mbolea
Wazazi wajibikeni kudhibiti utoro Shuleni - Senyamule