Dini katika madhehebu tofauti ikiwemo Uislam zimekuwa zikisisitiza suala la maadili, ambalo linajenga mahusiano mazuri kati ya mtu mmoja na mwingine huku zikizuia kutokea kwa ubaya miongoni mwa jamii na kusisitiza kutonyoosheqna vidole kwani kila mtu huwa na aibu yake.
Hayo yamesemwa na Sheikh Mussa Kundecha katika mahojiano ya kipindi cha Balagha Dar24 Media, ambapo ameelezea maadili jinsi yanavyoweza kukutanisha watu wa jamii tofauti.
Amesema, “na katika hili, hadithi ya Mtume Mohamed ambayo inatufundisha kuwa unapotaka kutaja aibu ya mtu hebu kumbuka kwanza aibu yako wewe na sio uikumbuke tu ni vyema uijue”.
Sheikh Kundecha ameongeza kuwa, “falsafa ya hapa ni kwamba uktaka kutaja aibu ya mwezio angalia aibu yako halafu jiulize kama mwanadamu aibu yanguu hii ikiwa inatolewa nitafurahi kiasi gani.”
“Ikiwa kama hutofurahi basi usione furaha kutoa aibu ya mwezio hili ni jambo laki maadili kwa kufanya hivyo maana yeke mwenye siri yake akijua wewe na yeye mahusiano yenu yanakuwa mabaya na hatuwezi kujua atachukua hatua gani baada ya kubaini umetoa siri yake,” amesema.