Muigizaji na mwanamuziki maaarufu nchini Ufaransa Jane Birkin amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76, nyota huyo mwenye asili ya Uingereza na Kifaransa alijulikana kwa uhusiano wake wa kikazi na wa kibinafsi na mwanamuziki Serge Gainsbourg.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Ufaransa mnamo Septemba 2021 alipatwa na ugonjwa wa kiharusi, na kumlazimisha kuhairisha kushiriki kwenye tamasha la filamu la Marekani

Alizaliwa London lakini alipata umaarufu akiimba kwa Kifaransa, na kuhamia huko katika miaka ya 1970. Vyombo vya habari vya Ufaransa viliripoti kwamba alikutwa amekufa nyumbani kwake huko Paris.

Uhusiano wake wa binafsi na wa kisanii na Gainsbourg ulimpa umaarufu kote ulimwenguni kufuatia wimbo wao wa kimataifa”Je t’aime… moi non plus” ambapo wimbo huo ulirekodiwa mnamo 1968, miezi kadhaa baada ya kukutana wakati wanatengeneza filamu , Slogan.

Wawili hao walikuwa pamoja kwa miaka 12 lakini walibaki marafiki baada ya kutengana, huku Gainbourg akiendelea kumwandikia Birkin nyimbo.

Sifa zake za uigizaji zilionekana kwenye filamu kama vile Blow Up ya mwaka wa 1966, Death on the Nile (1978) na Evil Under the Sun (1982).

Birkin pia alikuwa mwanamitindo na alionekana sana kama mwanamitindo, akihamasisha mkoba wa Birkin.

Aibu ya mwenzio ni yako - Sheikh Kundecha
Gara B awapa Vijana mbinu za kufanikisha ndoto