Kiungo Mshambuliaji wa Manchester City, Riyad Mahrez tayari amefikia makubaliano binafsi na klabu ya Saudi Arabia Al-Ahli katika dili la uhamisho ambalo linatarajiwa kuiona City ikipokea ofa ya kiasi cha pauni milioni 30 kwa winga huyo wa Algeria.
Riyad Mahrez anaweza kuwa mchezaji anayefuata kujiunga na Saudi Pro League msimu huu wa joto, hii ni baada ya raia huyo wa Algeria kupewa ofa ya pauni milioni 43 kwa mwaka pamoja na bonsai kwa mkataba wa miaka miwili.
Tangu ajiunge na City, Mahrez amefanikiwa kuichezea timu hiyo mechi 236 na kufunga mabao 78.
Winga huyo mwenye umri wa miaka 32 ambaye msimu uliopita alishinda mataji matatu ya kihistoria akiwa na City kwa sasa amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake na Manchester City.
Mahrez alionekana kutokuwa na furaha hususani mwishoni mwa msimu uliopita mara baada ya kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara, huku mwenyewe akiweka wazi anatamani kumalizia maisha yake ya soka huko Saudia.
Licha ya kuwa kwenye nafasi nzuri ya kujiunga na wababe hao wa Saudia, Mahrez bado anaonekana kuwa njia panda juu ya uamuzi wake wa kuondoka England baada ya miaka saba ya kuhudumu ndani ya kikosi cha Manchester City.