Rasmi imefichukua, uongozi wa mabingwa wa Europa, Sevilla wapo kwenye mpango wa kuinasa saini ya aliyekuwa kipa wa Manchester United, David De Gea mara baada ya miaka 12 ya kipa huyo kuhudumu nchini England.

Manchester United hivi karibuni walithibitisha kuondoka kwa De Gea katika klabu hiyo mara baada ya kushindwana katika mchakato wa kusaini mkataba mpya na kipa huyo na sasa Sevilla wanataka kumrejesha mlinda mlango huyo wa Hispania.

Mkataba wa De Gea na Manchester United ulimalizika mwishoni mwa mwezi Juni na alikuwa akiendelea na mazungumzo na mabosi wa timu hiyo hadi wiki iliyopita, lakini kutokana na kocha Erik ten Hag kuweka mkazo wa kuinasa saini ya kipa Andre Onana wa Inter Milan kuwa namba moja wake mpya, De Gea aliamua kuwa ni bora kutafuta klabu mpya, kukiwa na ofa mezani kutoka kwa Saudi Pro League.

Akizungumzia hilo De Gea alisema: “Sasa, ni wakati mwafaka wa kutafuta changamoto mpya ili kujisukuma tena katika mazingira mapya.”

De Gea anahitajika na Sevilla kama mbadala wa kipa wao, Yassine Bounou ambaye anahusishwa kuhitajika na Paris Saint-Germain na Bayern Munich msimu huu wa joto.

Robertinho afafanua safari ya Brazil
Kiungo fundi aupongeza uongozi Simba SC