Kocha Mkuu wa Kagera Sugar Mecky Mexime amemeweka wazi bado anahataji mastaa watakaokiboresha kikosi chake kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mexime ametoa kauli hiyo baada ya kikosi chake kuanza rasmi maandalizi jana Jumatatu (Julai 17) katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Kagera Sugar ni moja kati ya timu yenye ushindani katika Ligi Kuu Tanzania Bara, msimu uliopita ilimaliza nafasi ya 11 ikisalia katika ligi hiyo baada ya kupishana pointi nne na Mbeya City iliyoshuka kuifuata Polisi Tanzania na Ruvu Shooting.

Kocha Mexime amesema anaendelea kusaka wachezaji ambao wataongeza ushindani katika kikosi hicho msimu huu kutokana na ushindani ambao utakuwepo.

“Kila timu naona inafanya usajili hata mimi nafanya pia katika maeneo ambayo nahitaji hasa ni washambuliaji na mabeki kutokana na hali ya timu ilivyokuwa msimu uliopita,” amesema Mexime.

Amesema tayari kuna wachezaji ameanza kufanya nao mazungumzo na mambo yakikamilika watakuwa ndani ya kikosi hicho.

“Msimu uliopita timu yangu iliruhusu mabao 36 ya kufungwa na 23 ya kufunga hiyo inaonyesha kabisa kuna upungufu mahali na ndio maana tumekaa na wenzangu katika benchi la ufundi tunahakikisha tunaweka sawa,” amesema Mexime ambaye aliwahi kuwa kocha kuichezea Mtibwa Sugar na kuifundisha pia.

FIFA kuchelewesha dilila De Gea Uarabuni
Mkandarasi mradi wa maji aonja chungu ya janjajanja