Aliyekuwa mshambuliaji wa Geita Gold, Juma Luizio yupo mbioni kujiunga na klabu za JKT Tanzania au Mtib- wa Sugar kwa ajili ya kuzitumikia msimu ujao.

Luizio ambaye msimu uliopita alikuwa kwenye kikosi cha Geita Gold ameomba kuondoka licha ya kwamba alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja lakini tayari makubaliano yameshakamilika na mchezaji huyo yupo huru.

Mtu wa karibu na mchezaji huyo amesema kwamba Liuzio aliomba kuondoka ili akatafute changamoto sehemu nyingine na mabosi wa Geita walikubaliana naye.

“Liuzio kweli ni mchezaji huru halafu kwa sasa yupo kwao Morogoro, ninachojua ana ofa ya JKT Tanzania na Mtibwa,” kilisema chanzo hicho kwa kifupi.

Upande wa uongozi wa Geita Gold, msemaji wa klabu hiyo Samuel Dida alitaja orodha ya wachezaji ambao mikataba yao imeisha.

“Luizio ameomba kuvunjiwa mkataba, lakini wengine walioondoka ni mikataba yao imeisha.”

Wachezaji ambao mikataba yao imemalizika ni Danny Lyanga, George Wawa, Marc Arakaza, Jofrey Manyasi, Mussa Gadi, Shinobu Sakai na Jonathan Mwaibindi.

Harry Maguire kuibukia Chelsea?
Tengua teua ya Rais Samia imebeba maana kwa Taifa.