Wakati Arsenal kwa sasa ikiwa timu ya pili kuwa na kikosi ghali duniani, inaelezwa kwamba kocha wao, Mikel Arteta ameisuka timu hiyo kwa kutumia pauni 600m.

Arsenal kwa miaka minne ikiwa chini ya Arteta, imetumia takribani Pauni 600m katika usajili wake.

Ndani ya muda huo mfupi, Arteta amefanikiwa kuirudisha Arsenal katika ushindani ambapo msimu uliopita ilimaliza ligi nafasi ya pili na kupata tiketi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Katika hizo pauni 600m kwa miaka minne, Arsenal ya Arteta imetwaa Kombe la FA na Ngao ya Jamii, huku msimu ujao ikishiriki michuano ya UEFA baada ya kupita takribani miaka saba.

Arsenal kipindi hiki cha usajili wa majira ya joto, imefanikiwa kusajili wachezaji watatu ambao ni Declan Rice kwa pauni 105m, Jurrien Timber (pauni 38m) na Kai Havertz (pauni 65), huku kocha huyo akipewa pauni 250 za usajili.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 19, 2023
Dusan Vlahovic aingia anga za PSG