Mkoa wa Dar es Salaam umetajwa kuongoza kwa kuwa na Visimbuzi vingi zaidi nchini vinavyofikia 1,286,354, ikifuatiwa na Mkoa wa Arusha, Mwanza na Mbeya, huku watoa huduma wakishindana kwa utoaji wa huduma bora na si gharama.

Takwimu hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania – TCRA, Dkt. Jabir Bakari, wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo kwa mwaka wa fedha 2023-2024 na maendeleo ya sekta ya mawasiliano nchini.

Amesema, “Mkoa wa Arusha pia una jumla ya visimbuzi 275,449 , Mkoa wa Mwanza visimbuzi jumla 262,380 na Mbeya visimbuzi ni 208,924 hii ni mikoa ambayo inaongoza kuwa na visimbuzi vingi zaidi Nchini.”

Dkt. Jabir ameongeza kuwa Mkoa ambao una visimbuzi vichache ni pamoja na Mkoa wa Songwe wenye visimbuzi 1,357 huku mwenendo wa gharama za rejareja za kupiga simu kwa kutumia kifurushi ndani na nje ya mtandao kuanzia 2015 hadi sasa, zikiendelea kushuka na kufanya watu wengi kumudu gharama.

“Mwenendo wa gharama ndani na nje ya kifurushi zimeendelea kushuka na kukaribiana na hali hii imechochea shughuli nyingi za kiuchumi kuweza kufanyika kupitia mawasiliano ya simu ukilinganisha na hapo awali,” amesema.

Liverpool yamsaka kwa nguvu Kalvin Phillips
Kitayosce yaitaka saini ya Kocha wa Simba SC