Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar – ZEC, Jecha Salim Jecha.

Kifo cha marehemu Jecha kimetokea hii leo Julai 18, 2023 katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ambapo Rais Samia amesema amepokea taarifa za kifo cha marehemu Jecha kwa majonzi na masikitiko makubwa.

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar – ZEC, Jecha Salim Jecha.

Taarifa ya Mkurugenzi wa wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa, pia Rais Samia ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa kufuatia kifo cha Bernard William Mkapa (Mwenye Mkuti) ambae alikuwa ni kaka yake.

Aidha, Rais Samia amewaomba wanafamilia wote wawe na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na amewaombea marehemu wote wapumzike mahali pema peponi.

Waarabu wampa jeuri Kocha Newcastle United
Fikiri Elias kufanya kazi na Mwinyi Zahera