Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain wako tayari kuingia kwenye kinyang’anyiro na FC Bayern Munich kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane, msimu huu wa majira ya joto, kwa mujibu wa ESPN.

Mapema mwezi huu, ESPN iliripoti kwamba Kane anataka kujiunga na Bayern mabingwa wa Ligi Kuu Ujerumani, Bundesliga na hayuko tayari kuongeza mkataba wake na Spurs.

Lakini PSG pia wana nia ya kumsajili nahodha huyo wa England na vyanzo viliiambia ESPN kwamba klabu hiyo imekuwa kwenye mazungumzo na kaka wa Kane na wakala wake, Charlie kwa wiki kadhaa.

Mabingwa hao wa Ligue 1 wana nia ya kuleta mshambuliaji mwingine na pia wanawafuatilia Victor Osimhen wa Napoli na Randal Kolo Muani wa Frankfurt, vyanzo viliongeza.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, PSG wanaamini kwamba Kane anapendelea kwenda Bayern, lakini iwapo makubaliano hayatafikiwa, klabu hiyo ya Ufaransa itakuwa tayari kutoa fedha zaidi kwa Spurs na kujaribu kumshawishi mshambuliaji huyo kujiunga nao.

PSG wako tayari kutumia euro milioni 100 kumnunua mshambuliaji na kiasi hicho kinaweza kuongezeka iwapo Kylian Mbappé ataondoka na kujiunga na Real Madrid kwa ada kubwa ya uhamisho.

Klabu hiyo ya Ufaransa inapitia kipindi cha kuimarika baada ya Lionel Messi kuondoka na kujiunga na klabu ya MLS Inter Miami msimu huu wa majira ya joto.

Mkurugenzi wa michezo, Luis Campos ameimarisha maeneo mengine kwa kuwasajili Marco Asensio, Manuel Ugarte, Lucas Hernandez, Cher Ndour, Lee Kang-in pamoja na kocha mpya, Luis Enrique.

Bayern pia wameshuhudia ofa mbili zikikataliwa kwa Kane, lakini wanatarajiwa kutuma ofa ya tatu ya takriban euro milioni 90, am- bayo bado itashindwa kufikia thamani ya Spurs.

Wakati huohuo, meneja mpya wa Spurs Ange Postecoglou alisema amezungumza na Kane, ambaye atatimiza umri wa miaka 30 Julai 28, mwaka huu, kabla ya mechi yao ya kwanza ya kujiandaa na msimu mpya dhidi ya West Ham United nchini Australia.

“Nilikuwa na mazungumzo mazuri na Harry,” aliwaambia waandi- shi wa habari katika mkutano wake Jumatatu.

“Mazungumzo mazuri tu, nilijitambulisha, na tulizungumza zaidi juu ya klabu iko wapi na wapi anafikiria inaweza kuimarika.

“Sio maono maalum kwa mtu mmoja, ni kuhusu kundi na tumejipanga kikamilifu katika hilo tunataka kuona timu yenye mafanikio mwaka huu.”

Prof. Mkenda aitaka TCU kusimamia tafiti maeneo bobezi
Usajili wa Lilepo waigawa Young Africans