Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Qin Gang (57), hajaonekana hadharani tangu mwishoni mwezi uliopita (Juni) na kuzua tetesi juu ya uhusiano wake na mtangazaji maarufu wa televisheni ambaye walitangaza uchumba Juni 25, 2023.

Qin ambaye ni Mwanadiplomasia aliyeaminika na msaidizi wa karibu wa Rais Xi Jinping, aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Desemba mwaka jana, akitokea kwenye nafasi ya balozi wa China nchini Marekani na pia aliwahi kuwa balozi nchini Uingereza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Qin Gang (57) Picha ya EPA.

Mbali na ubalozi, Qin pia amepitia nyadhifa mbalimbali ndani ya Chama cha Kikomunisti cha China (CCP), alijenga jina kwa ujasiri wake katika masuala ya kidiplomasia, hasa mikutano yake na maofisa wa serikali katika nchi za magharibi.

Hata hivyo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China, Mao Ning alisema hana taarifa za kutoa huku hali ya kutoweka ghafla kwa maafisa wa ngazi za juu kukileta picha mbaya na kuzua mashaka zaidi miongoni mwa jamii.

Maandamano yasitisha huduma ya usafiri wa Reli
Mshambuliaji Azam FC anaswa Simba SC