Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi – CCM, Daniel Chongolo amewasili Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga, tayari kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika uwanja wa Mazoezi mjini humo.

Katika mkutano huo, pamoja na mambo mengine Chongolo ataelezea hatua kwa hatua usahihi wa makubaliano ya uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.

Lengo wa kuelezea suala hilo, ni kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa uwekezaji katika maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, uelimishaji huo pia utasisitiza juu ya uhakikishaji wa bandari hiyo kutoa huduma kwa viwango vya hali ya juu tofauti na ilivyo sasa.

Tamaa ya mafanikio chanzo matumizi Dawa za kulevya
Maandamano yasitisha huduma ya usafiri wa Reli