Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana, Dkt. Brayson Kiwelu amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pongezi kwa Mariam Mwakabungu (25), anayejitolea kukumbatia watoto njiti waliotelekezwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana.

Dkt. Kiwelu amesema ujumbe huo umetumwa na Rais Samia ambaye amekuwa mstari wa mbele katika huduma za mama na mtoto ambaye amemkabidhi Mariam kiasi cha Sh2 milioni.

Rais Samia ametuma ujumbe huo mara baada ya gazeti la Mwananchi kuripoti habari ya Mariam aliyesaida waliotelekezwa na mama zao ambapo alitoa Shilingi millioni 2 kumpatia mama huyo kwa kujitoa kwake na amewapongeza viongozi wa Wizara ya Afya na Amana kwa ubunifu na uthubutu mama huyo kuwa sehemu yao.

Amesema, “Rais ameshukuru sana msaada ambao mama huyu ameutoa na amewataka Watanzania kuendelea kujitoa kwa ajili ya kuhudumia wale wenye uhitaji.”

Mbaroni kwa kubaka, kutomasa watoto
Kuwa mpinzani sio kosa la jinai - Tundu Lissu