Wananchi wa Kijiji cha Migongo Wananchi wa Kijiji cha Migongo wameishukuru serikali kwa kumtua mama ndoo kichwani baada ya kukamilika kwa mradi wa maji katika eneo lao, utakaowahudumia jumla ya watu 14,242.

Waananchi hao wametoa shukrani zao mbele ya Wziri wa Maji, Jumaa Aweso ambaye walimpokea kwa shauku Kijinini Migongo wilayani Buhigwe, kutokana na eneo hilo kutokuwa na huduma ya Maji iliyowalazimu kwenda umbali mrefu kutafuta hitaji hilo muhimu.

Aidha, Waziri Aweso baada ya ukaguzi wa Mradi huo ameridhishwa na utekelezaji wake na kuwapongeza wahandisi wa maji RUWASA kwa kazi nzuri.

Mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi Billion 1.1 na umekamilika kwa asilimia 94 huku ukianza kutoa huduma ya maji Kwa wananchi wa Kijiji hicho cha Migongo.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 20, 2023
Mbaroni kwa kubaka, kutomasa watoto