Kocha Mkuu wa Chelsea, Mauricio Pochettino anapiga hesabu kunasa huduma ya beki Harry Maguire kabla dirisha hili la kiangazi halijafungwa.

Beki huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 30, anaweza kuachana na Manchester United dirisha hili baada ya kuvuliwa unahodha na kocha Erik ten Hag, Maguire aliyemwanzishwa mara nane Ligi Kuu England msimu uliopita na kitendo cha kuvuliwa unahodha ina maana hayupo kwenye mipango ya Ten Hag.

Maguire bado ana mkataba wa miaka miwili na kuna klabu kibao zinahitaji saini yake zikielezwa kwamba zinaweza kumudu mshahara wake wa Pauni 200,000 kwa juma.

Chelsea ni moja ya klabu hizo na Pochettino, aliyeteuliwa Juni, kwa muda mrefu amekuwa akivutiwa na beki huyo, Pochettino alionyesha kuvutiwa na Maguire miaka saba iliyopita alipokuwa akiinoa Tottenham Hotspur.

Kipindi hicho beki huyo wa kati alikuwa akikipiga Hull City na baadae akajiunga na Leicester City kwa ada ya Pauni 17 milioni mwaka 2017 kabla ya kutua Old Trafford kwa ada ya Pauni 80 milioni mwaka 2019.

Ishu ya Pochettino kuvutiwa na Maguire ilifichuliwa na Danny Rose, mmoja wa wachezaji wake wa zamani, ambaye alisema: “Nakumbuka tulicheza na Hull uwanjani White Hart Lane (Desemba 2016) na tulishinda 3-0.”

“Mauricio alikuwa kocha wetu na Harry alikuwa kila sehemu. Spurs nadhani walihitaji saini yake. Poch alionekana wazi kuhitaji saini yake.

Nilipokuwa nafanya naye mazoezi kwenye kikosi cha England, ilikuwa ngumu sana kupata mpira kutoka kwake. Ni mzuri kiasi hicho.”

Timu nyingine zinazomtaka Maguire ni Chelsea, West Ham, Tottenham na Newcastle United. Man United inaweza kukubali kumwachia kwa Pauni 50 milioni kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Chama, Ngoma wana shughuli nzito Uturuki
Ihefu FC wamtia pini Victor Akpan