Kikao cha Wajumbe wa Tume ya haki jinai, DPC na Wahariri wa Vyombo vya Habari, kimefanyika hii leo Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo mambo mbalimbali yamesemwa ikiwemo kuachiliwa kwa Mahabusu 2,240 tangu Rais Samia aingie madarakani.
Kikao hicho pia kimesema miongoni mwa watu walioachiliwa huru ni pamoja na Viongozi wa dini, Wanasiasa, watu mashuhuri na wananchi wa kawaida na kwamba lengo la Rais ni kushughulikia malalamiko ya muda mrefu ya wananchi kuhusu utoaji hakina.
Aidha, imearifiwa kuwa pia Mahakama za chini zimeanza kutoa tasfiri za kiswahili, ili wananchi wafahamu vizuri mwenendo wa kesi na kuanzishwa kwa Samia Legal Campaign ili kutoa msaada wa kisheria bure na kwamba mamlaka waliyopewa RC, DC kukamata yafuate sheria na yasitumike kuwaonea Wananchi.
Kwa nyakati tofauti, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Eliezer Feleshi, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki Jinai, Balozi Ombeni Sefue na Mgurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus walipata nafasi ya kuzungumza mbele ya Waandishi wa Habari ambao waliuliza pia maswali kadhaa.