Tume ya Haki Jinai imependekeza Viongozi wa Umma wanaotumia vibaya madaraka yao kuwaweka mahabusu wananchi kinyume cha sheria, kushtakiwa binafsi Mahakamani badala ya kuishirikisha Serikali.

Hayo yamebainishwa hii leo Julai 20, 2023 na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Eliezer Feleshi katika Kikao cha Wajumbe wa Tume ya haki jinai, DPC na Wahariri wa Vyombo vya Habari Ikulu jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, pia Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki Jinai, Balozi Ombeni Sefue alisema, “wakati tunazunguka kupata maoni ya Wananchi tuliulizwa mahali fulani ‘Hivi tuna Serikali ngapi?’ nikamwambia kwanini unauliza?.”

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Eliezer Feleshi.

“Akasema ‘Mimi najua kila Serikali ina Jeshi moja sasa hapa ukiamka asubuhi hujui utakamatwa na Jeshi lipi?, utakamatwa na Polisi, TAKUKURU, Watu wa misitu na wanyamapori, kwahiyo hiyo ndio dhana ya Wananchi,” alisimulia Balozi Sefue.

Hata hivyo ameongeza kuwa, “Tutoe wasiwasi kuhusu maliasili na misitu, kuna wanaopambana na Majangili wataendelea kuwa na unifomu na silaha kwa kadri ya uzito wa majukumu.”

Mahabusu wamuomba Hakimu Mbuzi wafanye sherehe
Rais Dkt. Samia awaachilia huru wafungwa 2,240