Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demnokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Tundu Lissu amesema aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ni Jambazi na endapo angeshitakiwa kwa makosa yote aliyowahi kuyatenda, basi angepaswa kuwa gerezani kwa maisha yake yote Duniani.

Lissu ameyasema hayo wakati akifanya Mahojiano maalum na Dar24 Media nyumbani kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kudai kuwa hayo si maneno yake bali imethibitishwa na vyombo vyenye mamlaka na alihukumiwa kwa kuyatenda makosa mbalimbali ya jinai.

Amesema, “wengine wanasema alifanya kwa utashi wa kisiasa, hakuna utashi wa kisiasa kwenye makosa ya jinai, wa kwetu walisingiziwa yeye hakusingiziwa na huko mtaani wako akina Sabaya wengi ambao kuna makosa mengine wameyafanya waziwazi.”

Hata hivyo Lissu ameongeza kuwa, “wapo watu watu ambao walikuwa wakiwafungulia watu mashitaka ya uongo na kuwanyang’anya mali akina DPP Mganga Biswalo, leo ni Jaji na ulimsikia mama anasema wananyang’anya watu hela wanazipeleka China watu wote hawa walifanya makosa ya jinai na wanapaswa kushughulikiwa kijinai.”

Manchester United yaichorea mstari Atalanta
Mahabusu wamuomba Hakimu Mbuzi wafanye sherehe