Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa mazingira Bunda Mkoani Mara, imeweka mkakati wa kupunguza upotevu wa Maji wa miaka mitatu ulioanza Mwaka 2020/2021 hadi Mwaka 2023/2024.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira – BUWSSA, Esther Gilyoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya mamlaka na mwelekeo wa utekelezaji wa Mwaka wa fedha 2023/2024 jijini Dodoma.

Amesema, “upotevu wa Maji Bunda Mkoa wa Mara kwa mwaka 2022/2023 umefika asilimia 36% na mkakati huu ambao tunao najua itaenda kutokomeza kabisa upotevu wa maji katika Wilaya ya Bunda, hivyo wananchi waendelee kutunza miradi yetu ya maji.”

Gilyoma ameongeza kuwa, BUWSSA imeandaa andiko la mradi kwaajili ya kukopa kuhakikisha upotevu wa Maji unapungua kwa kiasi kikubwa zaidi na kusema, “tumeandaa andiko kwaajili ya kukopa fedha kiasi cha Shilingi 815,000,0000 ili upotevu wa maji upungue kuanzia mwaka wa fedha 2023/2024.”

Hata hivyo, amesema Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Bunda haina huduma ya Majitaka, hivyo Magari ya Watu binafsi ambayo yanasimamiwa na halmashauri ya Mji wa Bunda ndiyo yatatumika katika kutoa huduma.

Afisa wa Polisi akamatwa na misokoto 40 ya Bangi
Ajali ya Ndege: Marubani JWTZ wanusurika kifo Bukoba