Klabu ya Ihefu FC imeendelea kujiweka sawa baada ya kukamilisha usajili wa kipa Hussein Masalanga na beki wa kushoto, Mpoki Mwakinyuke, ambao msimu uliopita walikuwa wakiichezea Ruvu Shooting, pamoja na Geofrey Manyasi aliyekuwa Geita Gold.

Masalanga na Mwakinyuke wamejiunga na timu hiyo wakitokea Ruvu Shooting baada ya kushuka daraja, huku Manyasi akimaliza mkataba wake ndani ya Geita Gold.

Chanzo kutoka eneo ambalo Ihefu FC imeweka kambi kimedokeza kwamba wachezaji hao tayari wameshajiunga na timu, huku wakisubiri kujiunga na wengine kwa ajili ya kuanza ratiba ya maandalizi ya msimu mpya.

“Kweli wachezaji hao wapo na wenzao wapya wakisubiri tu kutambulishwa na kuanza mazoezi ya pamoja, timu inaziba mapengo ili kikosi kiwe kizuri,” kimesema chanzo hicho.

Nje ya wachezaji hao, mwingine ambaye anatajwa kwamba ameshamalizana na Ihefu FC ni beki wa kushoto, Issa Rashid Baba Ubaya’ aliyekuwa Mtibwa Sugar na tayari ameshaaga kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

Wakati huo huo, Ihefu FC imeondokewa na wachezaji wake Nico Wadada, Yahya Mbegu na Andrew Simchimba.

Bondia Majiha amtamani Tonny Rashid
Mkate wenyewe umeoza - Odinga amjibu Ruto