Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya – DCEA, imesema Wazazi na walezi wanayo nafasi kubwa ya kusaidia mapambano ya Dawa za kulevya kwa kuzungumza na watoto wao juu ya madhara yanayoweza kuwapata endapo watajihusisha na jambo hilo.

Hayo yamebainishwa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya – DCEA, Aretas Lyimo wakati akiongea na Dar24 Media jijini Dar es Salaam kuhusu zoezi la utoaji wa elimu kwa jamii juu ya sheria zinazoongoza Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, madhara na aina ya Dawa za kulevya.

Sehemu ya Wazazi katika moja ya vikao kujadili mambo muhimu katika jamii. Picha ya Interpeace.

Amesema, wengi wa wanaotumia Dawa za kulevya ni watoto ambao wana wazazi na wengi wao wamekuwa hawachukui jukumu la kuwasimamia na kufahamu kile watoto wao wanachokifanya ili kuwagundua au kuwapa elimu ya kuwaepusha na jambo hilo haramu linalopoteza nguvu kazi ya Taifa, na kuharibu maisha ya Vijana.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya – DCEA, Aretas Lyimo.

Hata hivyo, Kamishna Lyimo amesema tayari wameweka mikakati mipya na kutumia ile iliyopo kwa kushirikiana na wizara ya Kilimo ili kuyabaini maeneo ambayo yamekithiri kwa kujihusisha na kilimo cha Bangi na Mirungi kama zao la biashara, ili kubaini mazao mbadala ya kuwaingizia kipato.

“Lakini pia tumeandaa muongozo wa ufundishaji ambao kupitia NGO’s, kupitia wadau wetu mbalimbali na Wizara ya Elimu basi Wanafunzi na jamii watakuwa na uelewa wa Dawa za kulevya na jinsi ya kuepukana nazo na madhara yake, kwasababu wengi wanaingia kwakuwa hawajui madhara yake,” amesema.

Gamondi atamba kutetea ubingwa Tanzania Bara
Kambi ya Uturuki yapandisha mzuka Simba SC