Maandamano ya siku tatu ya Wafuasi wa Azimio la Umoja chini ya Kinara wa Upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ambaye hakuonekana hadharani akisema alikuwa anaumwa yametamatika huku ikidaiwa kuwa Polisi wana shida kubwa kuliko Wananchi.

Wakizungumza kwa nyakati tofuti wanaandamaji hao wanadai kuwa kinachowafanya Polisi kutumia nguvu kubwa ni kuonesha hisia na kumaliza hasira zao kutokana na hali ngumu inayowakabili kiuchumi kuliko mwananchi wa kawaida.

Moja kati ya wandamanaji Richard Emorut na Kamau Gitonga wamesema, “na washukuru sheria inawalinda na pia wana silaha lakini tu kama hawana kitu au wawenazo na sisi tukuwe nazo aaah mazeee, wangetambua kwanini tuliitwanga wananchi wenye hasira kali, wana shida mingi ya uchumi wale kuliko sisi.”

Hata hivyo, Mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yamewakashifu maafisa wa Polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi kuwakabili waandamanaji, huku Serikali ya Kenya ikiwatetea kwa kusema walikuwa wanawajibika na Rais, William Ruto akisititiza kuwa wahalifu hawana nafasi katika jamii.

Alhaj Dkt. Mwinyi ahimiza uzingatiaji suala la elimu
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 22, 2023