Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Emmanuel Gabriel ‘Batgol’ amekiangalia kikosi cha sasa cha timu hiyo kilichosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano na kuitabiria makubwa kitaifa na kimataifa, huku akiwauma sikio mabosi wa klabu hiyo kuhakikisha tu wanahamisha wachezaji.

Batgol aliyekuwa kwenye kikosi kilichofika Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza 2003 kilichoivua ubingwa Zamalek ya amesema usajili Misri, wa wachezaji wapya kimeifanya Simba SC kuimarika na kilichobaki ni wachezaji kuwapa raha mashabiki uwanjani.

Simba SC imewasajili Willy Onana kutoka Rayon Sports ya Rwanda, Kramo Aubin aliyetokea ASEC Mimosas, beki Che Fondoh Malone (Coton-sport) na Fabrice Ngoma (Al Hilal), mbali na kumrejesha David Kamata (Duchu), huku ikielezwa Luis Miquissone dili lake likiwa freshi kwa sasa.

Kutokana na usajili huyo, Batgol amesema anaona Simba SC ikifika mbali kwani nyota wote waliosajili wanaonekana kuwa bora wakiungana na waliokuwapo na kitu muhimu wachezaji watazingatia watakachoelekezwa na benchi la ufundi.

“Kiukweli Mungu akiwajaalia wachezaji wakaenda kama vile tunavyowasikia huko na kuwashuhudia, naamini itakuwa timu nzuri, Simba SC ya safari hii ina utofauti wa usajili, viongozi wameamua,” amesema nyota huyo wa zamani wa Nazareti ya Njombe.

“Lakini kwa asilimia kubwa naamini viongozi wameamua kujitoa, imewakera hii miaka minne la muhimu wawajaze sumu wale wachezaji wawaambie jinsi ilivyo ili wasije wakatuletea tena yale yale,” amesema Mshambuliaji huyo aliyekipiga pia Tanzania Prisons.

Bernard Morrison: SKUDU waoneshe watanzania
Majimengi kukabidhiwa Gwanda Namungo FC