Hatimaye Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Msumbiji Jose Luis Miquissone amerejea Simba SC kama mchezaji huru, baada ya kuvunja mkataba na Mabingwa wa Soka Barani Afrika Al Ahly ya Misri.

Miquissone aliondoka Simba SC miaka miwili iliyopita akisajili Al Ahly, baada ya kuonesha uwezo mkubwa katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, akiifunga bao pakee na la ushindi katika mchezo wa Mzunguuko wa pili hatua ya Makundi msimu wa 2020/21.

Simba SC imemtambulisha rasmi mchezaji huyo kupitia vyanzo vyake vya habari, ikiwa ni tukio la kwanza kutangazwa baada ya kutambulishwa kwa jezi za msimu mpya za klabu hiyo jana Ijumaa (Julai 21) majira ya saa moja usiku.

Ujumbe alioambatana na picha ya utambulishi wa Miquissone katika vyanzo vya habari vya Simba SC umeandikwa: Amerudi anapostahili kuwepo. Karibu tena nyumbani, Luis Miquissone. #NguvuMoja

Bilioni za Mama: Tanga UWASA yaupiga mwingi Funguni
Obrey Chirwa apata chaka jipya Ligi Kuu