Uongozi wa Dodoma Jiji FC umeendelea kuwatambulisha nyota wao wapya ambapo kwa sasa umemtambulisha rasmi Meshack Abraham.

Nyota huyo ametokea Kagera Sugar baada ya mkataba wake kufika tamati na sasa anaungana na walima zabibu ambao mpaka sasa wamemtambulisha Simon Gustapha na Iddy Kipangwile.

Akizungumza Afisa Habari wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga alisema: “Tumekamilisha usajili wa nyota Meshack Abraham na ni moja ya wachezaji wazuri ambao wana uzoefu na ligi atakuja kufanya kazi kubwa uwanjani msimu wa 2023/2024.

“Tunafanya usajili wa wachezaji bora ambao watakuja kuiongoza timu yetu na kuweza kufikia malengo ambayo atakuweza kufika msimu uliopita, lakini kwa Sasa tunaangalia wachezaji wenye viwango vikubwana wenye ubunifu na ambao wanaweza kuhimili presha wakiwa uwanjani.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 23, 2023
Ahmed Ally: Hatubahatisha usajili 2023/24