Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Charles Ilanfya anatajwa kufikia makubaliano mazuri na Ihefu FC muda wowote atasaini mkataba mpya na kutangazwa.

Ilanfya msimu wa 2022/23 alikuwa anacheza Mtibwa Sugar alipokuwa akitimiza majukumu yake kwenye ligi.

Nyota huyo amecheza timu kadhaa kwenye soka la ushindani ikiwa ni pamoja na KMC FC, Mwadui FC na Simba SC.

Mtu wa karibu wa Ilanfya aliyefunga mabao sita kwenye ligi akiwa na Mtibwa Sugar amesema kuwa mshambuliaji huyo wamefikia makubaliano mazuri na Ihefu.

“Mpaka sasa ni sehemu nzuri ambayo wamefikia mchezaji na Uongozi wa Ihefu FC, kinachosubiriwa ni kusaini na kutambulishwa, ni hivyo tu basi,” imeeleza taarifa hiyo.

Ilanfya amesema: “Msimu mpya unakuja ninatambua na changamoto mpya ni muhimu hivyo wakati ukifika itafahamika wapi ambapo nitakuwa.”

PICHA: Siku ya Mwananchi yafunika Dar
Hasheem Ibwe: Azam FC itashangaza 2023/24