Kocha wa Majogoo wa Jiji ‘Liverpool’ Jurgen Klopp anataka Jordan Henderson na Fabinho waondoke haraka ili apate nafasi ya kutumia Pauni 80 milioni zake kuleta mastaa wapya wa kuchukua buti za viungo hao.

Kinda wa Southampton, Romeo Lavia mwenye umri wa miaka 19, na staa wa Crystal Palace, Cheick Doucoure mwenye umri wa miaka 23 ni wakali wawili waliopo kwenye rada za Kocha Klopp akitaka watue Anfield kwenda kupiga kazi kwa ajili ya msimu ujao. Na mpango wa Klopp ni kuwapata wawili hao kwa Pauni 40 milioni kwa kila moja.

Miamba hiyo ya Anfield, tayari imeshatumia Pauni 100 milioni kwenye usajili wa dirisha hili ilipowanasa viungo Alexis Mac Allister na Dominik Szoboszlai na sasa kocha Klopp anataka pesa za kuwauza Henderson na Fabinho zitumike kwenye kuleta wapya.

Henderson mwenye umri wa miaka 33, aliondoka kwenye kambi ya Liverpool ya huko Ujerumani kwenda kukamilisha uhamisho wake wa Pauni 12 milioni kwenda Saudia.

Harry Kane ailia KABUNYAU Tottenham Hotspur
Arsene Wenger apewa maua yake Arsenal