Moto mkubwa unaoendelea nchini Algeria wakati huu wa wimbi la joto kali umeua zaidi ya watu 30 na wengine 26 kujeruhiwa huku maelfu wakihamishwa katika maeneo athirika.

Wataalam toka idara ya maafa nchini humo wamesema, vipimo vya joto vilifikia nyuzi joto 48, za vipimo vya Celcius, katika baadhi ya maeneo ya Taifa hilo la Afrika ya Kaskazini, huku Wizara ya Mambo ya Ndani ikisema ilirekodi mioto 97 katika mikoa 16, inayosambazwa na upepo mkali.

Taarifa ya Wizara hiyo ya Mambo ya Ndani imeeleza kuwa, mioto hiyo iliua watu hao 34, wakiwemo wanajeshi 10, huku Watu 1,500 walihamishwa kutoka mikoa ya Bejaia, Bouira na Jijel iliyopo mashariki mwa mji mkuu Algiers.

Mikoa hiyo mitatu katika eneo la pwani ya Mediterranean nchini Algeria imeshuhudiwa kuwa na mioto mibaya zaidi, huku Rais Abdelmadjid Tebboune akitoa rambirambi zake kwa familia za waliofariki na tayari wafanyakazi wa zima moto 7,500 na malori 350 ya yanatumiwa yakisaidiana na ndege ili kukabiliana na moto huo.

Serikali kuizika pamoja miili 103 ya Waandamanaji
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 25, 2023