Mlinda Lango kutoka nchini Cameroon Andre Onana ameeleza kwa nini amechagua kuvaa jezi namba 24 akiwa Manchester United, akisema aliichukua kwa sababu ni tarehe yake ya kuzaliwa.

Uhamisho wa Onana kwenda Man Utd ulithibitishwa rasmi Julai 20, mwaka huu huku mlinda mlango huyo akiweka bayana kuhusu mkataba wa miaka mitano klabu hiyo ikisalia na chaguo kwa mwaka zaidi baada ya ‘Mashetani Wekundu’ hao kukubali kulipa pauni milioni 47.61 kwa Inter kwa ajili ya huduma yake.

Huku David de Gea akiachana na jezi namba moja baada ya kumalizika kwa mkataba wake pale Old Trafford, Onana alitarajiwa kurithi namba moja, cha kushangaza ni kwamba Mcameroon huyo badala yake aliamua kuchagua namba 24.

Akielezea uamuzi huo kwa MUTV, Onana alisema: “Naipenda hiyo namba. Ni siku yangu ya kuzaliwa. Tarehe yangu ya kuzaliwa. Kwangu ni nzuri, ni nzuri.

“Ninapenda jezi hii kwa sababu namba hii tumefanya mengi na natumaini itaendelea.”

Onana alivaa jezi namba 24 wakati alipokuwa Inter, huku Samir Handanovic akiwa na jezi namba moja, na pia aliivaa Ajax pia.

Onana alivaa jezi hiyo alipowasili klabuni hapo kwa mara ya kwanza na, kufuatia msimu mmoja usiopendeza akivaa nambari moja msimu wa 2017/18, alirejea kwenye namba yake ya jezi aliyoipenda zaidi kampeni iliyofuata.

Katika mahojiano yake ya kwanza pale Manchester United, Onana pia alijadili mtindo wake wa uchezaji na hisia zake za kwanza za mazoezi na wachezaji wenzake wapya.

“Nina raha sana. Nadhani jambo muhimu zaidi ni kutambua hali hiyo na ndivyo ninavyofanya mwenyewe, kusoma hali, haswa kile timu inahitaji katika wakati fulani.

“Tunapocheza kutegemea tunacheza na nani, wakati mwingine unamiliki mpira na wakati mwingine huna, hivyo kutoka hapo lazima uwe na akili na ujaribu kusaidia timu, kwa sababu muda mwingi kucheza na hawa wachezaji ni jambo la kushangaza.

“Nilikuwa na kikao change cha kwanza cha mazoezi nao na inashangaza ubora wa hapa, ni mzuri.”

Sifa tano za Mlinda Lango Mbrazil Simba SC
Gamondi aahidi furaha maradufu Young Africans