Kiungo kutoka nchini Ecuador, Moises Caicedo ameweka mambo hadharani na kufichua anaweza kutua Chelsea dirisha hili.

Kauli hiyo imekuja baada ya kiungo huyo kuondoa neno Brighton kwenye wasifu wake kwenye ukurasa wake wa Instagram. Caicedo, 21, amekuwa chaguo la kocha mpya wa Chelsea, Mauricio Pochettino katika usajili wa dirishi hili la majira ya kiangazi.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Ecuador amekuwa mmoja kati ya viungo matata kabisa kwenye Ligi Kuu England baada ya msimu mmoja katika klabu yake ya Brighton.

Na sasa anapanga kupiga hatua nyingine kwenye maisha yake kwa kuhama kutoka Amex ili kutua Stamford Bridge.

Hata hivyo, Brighton inaweka ngumu kumpiga bei mchezaji huyo licha ya kumwahidi kumruhusu aondoke kwenye dirisha hilo la majira ya kiangazo baada ya kugoma kumuuza Arsenal kwenye dirisha la Januari mwaka huu.

Chelsea imeshashuhudia ofa zake mbili zikikataliwa, ikiwamo ya Pauni 70 milioni. Brighton inamthaminisha Caicedo kuwa na thamani ya Pauni 100 milioni ikimtumia Declan Rice, aliyesajiliwa kwa Pauni 105 milioni na Arsenal akitokea West Ham United kama kigezo chao kikubwa.

Caicedo hafurahishwi na kitendo cha Brighton kuweka ngumu kumuuza na ndiyo maana ameliondoa jina la timu hiyo kwenye wasifu wake katika ukurasa wa Instagram.

Kocha wa Brighton, Roberto De Zerbi alisema mchezaji huyo hauzwi kwenda timu yoyote katika dirisha hili la usajili labda kama tu kutakuwa na timu itakayokuwa tayari kulipa kiwango cha pesa kinachotakiwa na Mwenyekiti wa Brighton, Tony Bloom.

Morrison akaribia Singida Fountain Gate
CAF: Simba SC kwenda Namibia au Zambia