Bosi wa Singida Fountain Gate, Japhet Makau amesema usajili wa Benard Morrison ni suala la muda tu na mashabiki wakae kwa kutulia kwani mambo mazuri yanakuja zaidi msimu huu.

Morrison alipewa Thank You na Young Africans na inadaiwa tayari amemalizana na SFG kwa ajili ya kuitumikia msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na mashindano ya kimataifa ambapo watashiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Makau amesema kuwa: “Ishu ya Morrison tusubiri Agosti 2, ambapo tutatambisha kikosi chetu Kuhusu usajili wa wachezaji wapya akiwemo beki wa zamani wa Simba, Joash Onyango raia wa Kenya amesema;

“Kuna tofauti timu moja na timu nyingine, huwezi kusema mchezaji kama Onyango ameachwa,

“Sisi tuna imani nae na atafanya vizuri na atacheza kwa jinsi ambavyo kocha atamtumia, naamini wachezaji tuliowasajili wanaenda kufanya vizuri kwenye timu yetu.”

“Tutacheza Arusha ambako ndiko timu imeweka kambi, tutaenda kucheza Singida Agosti 2 mwaka huu katika siku yetu na tutaenda Tanga kucheza mechi ya Ngao ya Jamii,” amesema Makau.

Kuhusu maandalizi ya timu hiyo, Makau amesema yanaendelea vizuri jijini Arusha na wamepanga kutambulisha majembe yao Agosti 2 mwaka huu katika sherehe zinazotarajiwa kufanyika katika Uwanja Liti mkoani Singida.

“Unapofanikiwa unatengeneza ushindani mkubwa msimu unaofuata washindani wanakuangalia kwa umakini tumejipanga na malengo yetu ni kuwa katika nafasi tatu za juu.”

CAF: Azam FC yapelekwa Ethiopia, Singida FG Zanzibar
Moises Caicedo ajisogeza Stamford Bridge